Jeremiah 48

Ujumbe Kuhusu Moabu

1 aKuhusu Moabu:

Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa.
Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa;
Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa.

2 bMoabu haitasifiwa tena;
huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake:
‘Njooni na tuangamize taifa lile.’
Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa;
upanga utakufuatia.

3 Sikiliza kilio kutoka Horonaimu,
kilio cha maangamizi makuu na uharibifu.

4 Moabu utavunjwa,
wadogo wake watapiga kelele.

5 cWanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi,
wakilia kwa uchungu wanapotembea,
kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu,
kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.

6 dKimbieni! Okoeni maisha yenu,
kuweni kama kichaka jangwani.

7 eKwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu,
ninyi pia mtachukuliwa mateka,
naye Kemoshi
Kemoshi alikuwa mungu wa Wamoabu.
atakwenda uhamishoni,
pamoja na makuhani wake na maafisa wake.

8 gMharabu atakuja dhidi ya kila mji,
wala hakuna mji utakaookoka.
Bonde litaangamizwa na uwanda utaharibiwa,
kwa sababu Bwana amesema.

9 hWekeni chumvi kwa ajili ya Moabu,
kwa kuwa ataangamizwa;
miji yake itakuwa ukiwa,
pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake.


10 i“Alaaniwe yeye afanyaye kazi ya Bwana kwa hila!
Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu!


11 j“Moabu amestarehe tangu ujana wake,
kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake,
haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine,
hajaenda uhamishoni.
Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo,
nayo harufu yake haijabadilika.

12 Lakini siku zinakuja,”
asema Bwana,
“nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia,
nao watamimina;
wataacha magudulia yake yakiwa matupu
na kuvunja mitungi yake.

13 kKisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi,
kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu
walipotegemea mungu wa Betheli.
Betheli ina maana ya Nyumba ya Mungu; lakini pia ni mahali ambapo Mfalme Yeroboamu alisimamisha moja ya sanamu za ndama ili kuabudiwa; nyingine aliiweka huko Dani ( 1Fal 12:29-33 ).


14 m“Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa,
watu jasiri katika vita’?

15 nMoabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa,
vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,”
asema Mfalme, ambaye jina lake
ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.

16 “Kuanguka kwa Moabu kumekaribia,
janga kubwa litamjia kwa haraka.

17 oOmbolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka,
ninyi nyote mnaojua sifa zake,
semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu,
tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’


18 p“Shuka kutoka fahari yako
na uketi katika ardhi iliyokauka,
enyi wenyeji wa Binti wa Diboni,
kwa maana yeye aangamizaye Moabu atakuja dhidi yako,
na kuangamiza miji yako iliyozungushiwa maboma.

19 qSimama kando ya barabara na utazame,
wewe unayeishi Aroeri.
Muulize mwanaume anayekimbia
na mwanamke anayetoroka,
waulize, ‘Kumetokea nini?’

20 rMoabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjavunjwa.
Lieni kwa huzuni na kupiga kelele!
Tangazeni kando ya Arnoni
kwamba Moabu ameangamizwa.

21 sHukumu imefika kwenye uwanda wa juu:
katika Holoni, Yahasa na Mefaathi,

22 tkatika Diboni, Nebo
na Beth-Diblathaimu,

23 ukatika Kiriathaimu, Beth-Gamuli
na Beth-Meoni,

24 vkatika Keriothi na Bosra;
kwa miji yote ya Moabu,
iliyoko mbali na karibu.

25 wPembe
Pembe hapa ni ishara ya nguvu.
ya Moabu imekatwa,
mkono wake umevunjwa,”
asema Bwana.


26 y“Mlevye,
kwa kuwa amemdharau Bwana.
Moabu na agaegae katika matapishi yake,
yeye na awe kitu cha dhihaka.

27 zJe, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa?
Je, alikamatwa miongoni mwa wezi,
kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau
kila mara unapozungumza juu yake?

28 aaOndokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba,
enyi mnaoishi Moabu.
Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chake
kwenye mdomo wa pango.


29 ab“Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu:
kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno,
kiburi chake na ufidhuli wake,
na kujivuna kwa moyo wake.

30 Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,”
asema Bwana,
“nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote.

31 acKwa hiyo namlilia Moabu,
kwa ajili ya Moabu yote ninalia,
ninaomboleza kwa ajili
ya watu wa Kir-Haresethi.

32 adNinalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo,
enyi mizabibu ya Sibma.
Matawi yako yameenea hadi baharini;
yamefika hadi bahari ya Yazeri.
Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoiva
na mizabibu yako iliyoiva.

33 aeShangwe na furaha vimetoweka
kutoka bustani na mashamba ya Moabu.
Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo;
hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe.
Ingawa kuna kelele,
sio kelele za shangwe.


34 af“Sauti ya kilio chao inapanda
kutoka Heshboni hadi Eleale na Yahazi,
kutoka Soari hadi Horonaimu na Eglath-Shelishiya,
kwa kuwa hata maji ya Nimrimu yamekauka.

35 agNitakomesha wale wote katika Moabu
watoao sadaka mahali pa juu,
na kufukiza uvumba kwa miungu yao,”
asema Bwana.

36 ah“Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi;
unaomboleza kama filimbi kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.
Utajiri waliojipatia umetoweka.

37 aiKila kichwa kimenyolewa
na kila mwenye ndevu zimekatwa;
kila mkono umekatwa
na kila kiuno kimefunikwa kwa nguo ya gunia.

38 ajJuu ya mapaa yote katika Moabu
na katika viwanja
hakuna kitu chochote isipokuwa maombolezo,
kwa kuwa nimemvunja Moabu
kama gudulia ambalo hakuna mtu yeyote anayelitaka,”
asema Bwana.

39 “Tazama jinsi alivyovunjikavunjika!
Jinsi wanavyolia kwa huzuni!
Tazama jinsi Moabu anavyogeuka kwa aibu!
Moabu amekuwa kitu cha kudhihakiwa,
kitu cha kutisha kwa wale wote
wanaomzunguka.”

40 akHili ndilo asemalo Bwana: “Tazama! Tai anashuka chini,
akitanda mabawa yake juu ya Moabu.

41 alMiji itatekwa na ngome zake
zitatwaliwa.
Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu
itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa.

42 amMoabu ataangamizwa kama taifa
kwa sababu amemdharau Bwana.

43 anHofu kuu, shimo na mtego vinawangojea,
enyi watu wa Moabu,”
asema Bwana.

44 ao“Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu
ataanguka ndani ya shimo,
yeyote atakayepanda kutoka shimoni,
atanaswa katika mtego,
kwa sababu nitaletea Moabu
mwaka wa adhabu yake,”
asema Bwana.


45 ap“Katika kivuli cha Heshboni,
wakimbizi wamesimama pasipo msaada,
kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni,
mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni;
unaunguza vipaji vya nyuso za Moabu,
mafuvu yao wenye kujivuna kwa kelele.

46 aqOle wako, ee Moabu!
Watu wa Kemoshi wameangamizwa;
wana wako wamepelekwa uhamishoni
na binti zako wamechukuliwa mateka.


47 ar“Lakini nitarudisha mateka wa Moabu,
katika siku zijazo,”
asema Bwana.

Huu ndio mwisho wa hukumu juu ya Moabu.
Copyright information for SwhKC